Baadhi ya Matukio kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Roma, Italia, Machi 2019

 • Tarehe 24 na 25 Oktoba 2018, jijini Rome kulikuwa na Mkutano wa Italya-frika ambao ulihudhuriwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga na Mheshimiwa Balozi Madafa. Mkutano huo ulihusu mahusiano ya Kuchumi kati ya Italy na nchi za Afrika. Pichani Mheshimiwa Waziri Mahiga anaonekana akijadili jambo na baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo.
 • Kwa jitihada za Mheshiwa Balozi George Madafa, Bodi ya Utalii Tanzania imetoa kibali cha kuwa na Mabalozi wawili wa hiari wa Utalii nchini Italy. Pichani wanaonekana Mabalozi hao ambao kulia kabisa ni Bi. Judith Mushi na wa tatu kulia ni Bi. Anna Mrio pamoja na Mheshimiwa Waziri Mahiga. Ubalozi hushirikiana na Mabalozi hao wa hiari katika kuitangaza Tanzania na kuitafutia watalii.
 • Tarehe 13 Desemba 2018, Kamishna Mkuu wa Kuzuia Madawa ya Kulevya nchini ndugu Rogers Siyanga alifika Ubalozini alipokuwa nchini Italy kwenye mafunzo ya muda mfipi. Pichani anaonekana Bwana Siyanga na mtaalamu aliyefuatana naye walipofika Ubalozini kumsalimia Mheshimiwa Balozi Madafa.
 • Balozi wa Tanzania nchini Italy ana ushirikiano mzuri na Mabalozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC). Katika kudhihirisha ushirikiano huo mzuri, pichani anaonekana Mheshimiwa Balozi wa Burundi nchini Italy Bibi Nisubile, akiwa ni mmoja kati ya Waheshimiwa Mabalozi wengi waliofika Ubalozini kusaini kitabu cha rambirambi wakati wa ajali ya MV Nyerenyere Kisiwani Ukerewe.
 • Tarehe 13 na 14 February 2019 katika Makao Makuu ya Mfuko wa Maendeleo wa Kilimo Duniani (IFAD) kulikuwa na Mkutano wa Baraza la Magavana ambalo Mheshimiwa Japhet Hasunga - Waziri wa kilimo na Chakula alihudhuria. Pichani wanaonekana Mheshimiwa Waziri huyo, Mheshimiwa Balozi na msaidizi wa Waziri wakati wa Mkutano huo. Mheshimiwa Waziri pia alipata fursa ya kutembelea Makao makuu ya Shirika hilo ambako alijulishwa kwamba Tanzania imetengewa Dola Milioni hamsini na nane za maendeleo ya Kilimo katika kipindi cha miaka cha miaka mitatu ijayo.
 • Tarehe 01 Machi 2019, Balozi aliwatembelea wamiliki wa Kampuni ya Protcno ambayo imeunda Mitambo ya kutolea chumvi kwenye Maji iliyoagizwa na Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Morogoro (MOROWASA) kwa ajili ya kufungwa katika mji wa Gairo.
 • Pichani ni Mheshimiwa Balozi George Madafa akiwa na wamiliki wa Kampuni ya Protecno ambao ni Bwana Lorenzo Belbusti na Bwana Jacopo Belbusti. Kampuni hiyo hutengeneza Mitambo ya kuondolea chumvi kwenye Maji.
 • Mheshimiwa Balozi akikagua mmoja kati ya Mitambo mitatu (3) ya kuondolea chunvi kwenye Maji iliyotengezwa na Kiwanda cha Protecno kwa ajili ya Mji mdogo wa Gairo.
 • Mabalozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Italy wamo katika maandalizi ya Mkutano wa uwekezaji kati ya wafanyabiashara wa Italy na wa nchi zao unaotarajia kufanyika mwezi April 2019. Pichani anaonekana Mheshimiwa Balozi wa Uganda nchini Italy Bibi Elizabeth Napoyek wakijadiliana mipango ya Mkutano huo ofisini kwa Mheshimiwa Balozi Madafa.
 • Mheshimiwa Balozi Madafa katika majadiliano na Kampuni iitwayo TMT iliyopo Ascoli Piceno Pwani ya Mashariki ya Italy inayojihushisha na uundaji wa mabodi na matenki ya magari na pia uzoaji wa kisasa wa taka ngumu katika miji mikubwa. Kampuni hiyo inataka kuja kuwekeza nchini Tanzania. Pichani anaonekana Mheshimiwa Balozi Madafa na mwenyeji wake katika eneo hilo Bibi Anna Minja katika Mkutano wa kwanza na mwenye Kampuni hiyo Mhandisi Alfredo Spinozzi wa tatu kutoka kushoto akiwa na wasaidizi wake Bi Daniela na Bwana Gino Lama.
 • Mheshimiwa Balozi Madafa akiwa katika majadiliano na Kampuni ya TMT nchini Italia.