Rais Mstaafu wa Kenya Mzee Daniel arap Moi alikuwa Rais wa pili wa Kenya kutoka mwaka 1978 mpaka 2002. Alikuwa Rais kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa nchi wakati huo Mzee Jomo Kenyatta. Aliaga dunia akiwa kwenye matibabu katika hospitali ya Nairobi tarehe 4 Februari 2020 akiwa na umri wa miaka 95.